WAZIRI LUKUVI AWASILI MKOANI TANGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa (katikati) alipokutana na
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela (wanne kulia) na Mkuu wa Mkoa
wa Manyara Mhe. Joel Bendera (watatu kushoto).

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.
Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera
wakiwasikiliza wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi katika kutatua mgogoro
wa mpaka unaoikabili mikoa hiyo.

Wawakilishi wa wakazi wa kata ya
Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiongozwa
na Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi (wasita Kulia) walipokutana
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi,

Wawakilishi wa wakazi wa kata ya
Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto
wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kukutana nae.

Eneo la Mji wa Lushoto ulioko mkoani Tanga.
……………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua
migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana
nayo.
Katika ziara hii Waziri Lukuvi
leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo
kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi
iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia
ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo
la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu
uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya
ziara yake mkoani Tanga.
Ikumbukwe mnamo tarehe 18
Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara Wilayani
Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo
kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa
kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa
kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja
sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu
wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao
vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Aidha, wawakilishi wa wakazi wa
kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto
walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi
yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la
Le-Mash Enterprises Limited.
Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza
malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea
hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu
ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
No comments