PSG kuvunja rekodi kwa kumnunua Neymar pauni milioni 196
MARCO Verratti, Ousmane Dembele na
Kylian Mbappe watakuwa kwenye mawindo ya Barcelona ikiwa timu hiyo itampoteza Neymar
anayetajwa kutakiwa na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa Daily Mail.
Taarifa zilizokuwepo awali zilitaja
vigogo wawili wa England, Manchester United na Chelsea walikuwa wakihitaji
huduma ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, lakini zilijitoa baada ya taarifa
ya pauni milioni 196.
Klabu hizo zililalamika kwamba, PSG inajiamini
kuwa na nafasi ya kuinasa saini ya Neymar na kumpeleka Ufaransa, wakati baba
mnzazi wa nyota huyo akivuta subira mazungumzo na klabu yake.
Ingawa, ilishindwa kumsajili msimu
uliopita kutokana na mambo yaliyojitokeza, imekuwa kimya kuhusu hatma yake.
Kwa mujibu wa GloboEsporte, Neymar
aliwaambia wachezaji wenzake kutoka Brazil, Marquinhos, Lucas Moura, Thiago
Silva na Dani Alves kwamba, ataungana nao Paris msimu ujao.
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
No comments