ALIYEKUWA Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais Kazi maalum katika Serikali ya awamu ya tano, Profesa Mark
Mwandosya amesikitishwa na kifo cha mke wa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe (47) na kuelezea namna
alivyochangia kuwauguza mwaka 2011/2012.
Profesa Mwandosya
ameyasema hayo juzi wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya
mazishi iliyofanyika katika makaburi ya familia nyumbani kwa Mwakyembe, Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Mwandosya amesema kifo
cha Linah Mwakyembe kinahuzunisha kutokana na ukweli kuwa aliyekuwa anapaswa
kutangulia mbele ya haki ni Dk. Mwakyembe pamoja nay eye Profesa Mwandosya
kutokana na jinsi alivyoshiriki kuwauguza pindi walivyoumwa na kulazwa nchini
India mwaka 2011 hadi mwaka 2012.
Amesema mwaka 2011
alipatwa na ugonjwa ambao ulimlazimu kukimbizwa India ambapo akiwa huko
alimtaarifu Dk. Mwakyembe kuwa amefika salama kwenye matibabu lakini alipokea
taarifa kuwa nae anaumwa sana na yupo nchini India akiwa Hospitali tofauti.
AMwandosya amesema pamoja na
kulazwa katika Hospitali tofauti lakini wake zao, mke wake, Lucy na Linah walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara na kuimbiana nyimbo
zenye kuwafariji waume zao kwa njia za simu, jambo ambalo lilikuwa likiwapa
faraja na hatimaye kupona.
Ameongeza kuwa kutokana
na faraja kutoka kwa marehemu ilichangia wao kupona haraka jambo ambalo limechangiwa Linah kuwa mcha Mungu, alikuwa na upendo mkubwa kwa jamii
na wananchi wakiwa na upendo kwake, ambapo akiwa jijini Dar es salaam amekuwa ni
mzee wa kanisa la Kunduchi.
Kwa upande wake aliyekua
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema mafanikio
aliyonayo sasa yametokana na juhudi za familia za Profesa Mwandosya na Dk.
Mwakyembe akiwemo marehem Linah Mwakyembe.
Amesema marehemu
alishiriki kikamilifu katika kumuuguza mume wake wakati yuko katika wakati
mgumu, jambo ambalo wengi walidhani Dk. Mwakyembe anaweza asipone lakini hali
imebadilika aliyekuwa mzima ndiye anapoteza uhai.
Dk. Mwakyembe amewashukuru waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza marehemu mkewe na
kwamba umati mkubwa uliojitokeza umeonesha upendo mkubwa sana kwake.
Amesema marehem mke wake
alikuwa akisumbuliwa na saratani ya titi na kwamba, aliweka nadhiri kuwa siku
akipona ataanzisha kitu ambacho kitasaidia wanawake wengine kuwaokoa kutokana
na kuugua magonjwa ya saratani ya titi, lakini kabla hajatimiza hilo amepatwa na
umauti, familia italifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment