Header Ads

ad

Breaking News

Mwandosya atoa neno zito kifo cha mke wa Mwakyembe



 
Profesa Mark Mwandosya akimfariji Dk. Harrison Mwakyembe aliyefiwa na mkewe, Linah wakati wa maandalizi ya mazishi yake kijijini kwao Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya.  Kushoto mke wa Profesa Mwandosya, Lucy.
Venance Matinya, Kyela.

ALIYEKUWA Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Kazi maalum katika Serikali ya awamu ya tano, Profesa Mark Mwandosya amesikitishwa na kifo cha mke wa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe (47) na kuelezea namna alivyochangia kuwauguza mwaka 2011/2012.

Profesa Mwandosya ameyasema hayo juzi wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya familia nyumbani kwa Mwakyembe, Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Mwandosya amesema kifo cha Linah Mwakyembe kinahuzunisha kutokana na ukweli kuwa aliyekuwa anapaswa kutangulia mbele ya haki ni Dk. Mwakyembe pamoja nay eye Profesa Mwandosya kutokana na jinsi alivyoshiriki kuwauguza pindi walivyoumwa na kulazwa nchini India mwaka 2011 hadi mwaka 2012.

Amesema mwaka 2011 alipatwa na ugonjwa ambao ulimlazimu kukimbizwa India ambapo akiwa huko alimtaarifu Dk. Mwakyembe kuwa amefika salama kwenye matibabu lakini alipokea taarifa kuwa nae anaumwa sana na yupo nchini India akiwa Hospitali tofauti.

AMwandosya amesema pamoja na kulazwa katika Hospitali tofauti lakini wake zao, mke wake, Lucy na Linah walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara na kuimbiana nyimbo zenye kuwafariji waume zao kwa njia za simu, jambo ambalo lilikuwa likiwapa faraja na hatimaye kupona.

Ameongeza kuwa kutokana na faraja kutoka kwa marehemu ilichangia wao kupona haraka jambo ambalo limechangiwa Linah kuwa mcha Mungu, alikuwa na upendo mkubwa kwa jamii na wananchi wakiwa na upendo kwake, ambapo akiwa jijini Dar es salaam amekuwa ni mzee wa kanisa la Kunduchi.

Kwa upande wake aliyekua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema mafanikio aliyonayo sasa yametokana na juhudi za familia za Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe akiwemo marehem Linah Mwakyembe.

Amesema marehemu alishiriki kikamilifu katika kumuuguza mume wake wakati yuko katika wakati mgumu, jambo ambalo wengi walidhani Dk. Mwakyembe anaweza asipone lakini hali imebadilika aliyekuwa mzima ndiye anapoteza uhai.

Dk. Mwakyembe amewashukuru waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza marehemu mkewe na kwamba umati mkubwa uliojitokeza umeonesha upendo mkubwa sana kwake.

Amesema marehem mke wake alikuwa akisumbuliwa na saratani ya titi na kwamba, aliweka nadhiri kuwa siku akipona ataanzisha kitu ambacho kitasaidia wanawake wengine kuwaokoa kutokana na kuugua magonjwa ya saratani ya titi, lakini kabla hajatimiza hilo amepatwa na umauti, familia italifanyia kazi.


No comments