MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA UGANDA WAKUTANA NA MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA TANZANIA
Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao baina ya Makamishina wa Tume ya
Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge
la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao
baina ya Makamishina hao ambacho lengo kubwa lilikuwa ni kubadilishana
uzoefu wa utedaji kazi kiliongozwa na Zungu kwa niaba ya Spika wa
Bunge, Job Ndugai ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa
Bunge la Tanzania. Makamishina hao wa Bunge la Uganda wapo nchini kwa
ziara ya Kibunge ya siku mbili.

Kiongozi
wa Msafara Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe
Cecilia Ogwal (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa
Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge
Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge mbaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bunge la
Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akizungumza wakati wa kikao baina ya
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa
Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge
Jijini Dar es Salaam.
Makamishina
wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya
Utumishi wa Bunge la Tanzania (waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa
pande zote mbili katika picha ya pamoja mara baada ya kikao.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
No comments