Header Ads

ad

Breaking News

Federer atwaa taji la Wimbledon mara ya nane

            Roger Federer mshindi mara nane wa michuano ya wazi ya Wimbledon. (Getty Images)
 
Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo tenesi duniani, Roger Federer ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji la michuano ya Wimbledon, kwa mara nane.



Federer ametwaa taji hilo la Grand Slam baada ya kumshinda mpinzani wake, Marin Cilic, kwa jumla ya seti tatu.

Katika seti ya kwanza bingwa huyu wa kihistoria alishinda 6-3, 6-1 na 6-4, katika mchezo uliochezwa kwa muda wa saa 1:41.

Hili ni taji la 19 la Grand Slam, kwa mchezaji huyu raia wa Switzerland, na kuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi ya England.

1 comment:

  1. Wannit to watch Wimbledon online for free and came to this link. Watch Wimbledon on Kodi finally I can watch it for free.

    ReplyDelete