ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA GARI BARABARANI
Askari wa usalama barabarani "trafiki" mkoani Tabora amefariki dunia
baada ya kugongwa na gari wakati akitekeleza majukumu yake.
Askari huyo aliyefahamika kwa jina E.51 Koplo Aswile Ambwene amefariki
dunia jana asubuhi ya saa 12:30 akiwa kazini eneo la barabara ya
Sikonge, kijiji cha Kipalapala kwa Chief, Kata ya Itetemia, mkoani
Tabora.
Mauti ya askari huyo yalisababishwa na gari lenye namba za usajili 564
ALG aina ya Isuzu likiendeshwa na dereva Hasan Husein-Kiula mwenye umri
wa miaka 36. Gari hilo lilikuwa likitokea Mpanda kwenda Kahama likiwa
limepakia magunia ya mahindi.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo alieleza kuwa, Hassan dereva wa
gari hilo alisimamishwa barabarani na askari mwenye namba G.4246
Konstebo Abuu, lakini dereva huyo aligoma kusimama na kusababisha
kumgonga askari namba E.51 Koplo Aswile Ambwene ambaye alipoteza maisha
papo hapo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Milambo Jeshini mkoani Tabora.
www.malunde.com
No comments