Header Ads

ad

Breaking News

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MOSHI KWENYE MSIBA WA NDESAMBURO,VIONGOZI WA CHADEMA WAKIPOKEA MWILI WA MAREHEMU

  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo  katika viwanja vya Majengo mkoani hapa.
Ndesamburo alifariki wiki iliyopita wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mwili wa Ndesamburo aliyeliongoza Jimbo la Moshi Mjini kwa miaka 15, akiwa Mbunge,unaagwa katika viwanja hivyo na saa 10 jioni ulipelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wabunge na viongozi wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo, wakiungana na mamia ya wafuasi na wakazi wa mikoa ya Kaskazini.
Matukio mbalimbali kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye msiba wa Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki hivi karibuni mkoani humo, Marehemu Ndesamburo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini utaagwa kwenye uwanja wa Majengo kuanzia leo na kesho na kisha kuzikwa mkoani humo haya ni matukio kadhaa ya picha za matukio yanayoendelea katika msiba huo.
Baadhi ya wa vijana waendesha bodaboda wakijiandaa kwa ajili ya maandamano maalum wakati mwili wa marehemu utakapokuwa akipelekwa kwenye uwanja wa Majengo.
Gari Maalum litakalochukua mwili wake.
Eneo la Uwanja wa Majengo ambalo ndipo shughuli za kuaga mwili zitafanyika likiwa limepambwa tayari kwa shughuli hizo. CLEO24NEWS

No comments