Yanga kuivaa AFC Leopards nusu fainali SportiPesa Super Cup

MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, wametinga nusu fainali ya michuano ya SportiPesa Super Cup baada ya kuitoa Tusker FC ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2, katika mchezo uliocpigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Baada ya ushindi huo, Yanga sasa itacheza na AFC Leopards iliyoiondosha Singida United kwa ushindi wa penalti 5-4.
Timu hizo zitaumana katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Juni 8, mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Uhuru.
Katika dakika 90 za mchezo, timu hizo zimetoka suluhu, hivyo zikaingia kwenye hatua ya kupigiana penalti.
Yanga dakika ya 34 kupitia kwa Mahadhi, wangeweza kupata bao lakini walishindwa kuelewana na Obrey Chirwa kwa kupiga shuti lililookolewa na mabeki na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Yanga waliopata penalti ni nahodha Nadir Haroub 'Canavaro',
Chirwa, Maka Mwakaluka na Said Musa wakati kwa Tusker ni Asike Eugen na
Noah Wafula.







No comments