Forbes: Wasanii na wachezaji matajiri zaidi duniani watajwa
![]() |
| Beyonce na JK Rowling ndio wanawake pekee katika 10 waliopata pesa nyingi zaidi |
Jarida la Forbes limetoa orodha ya watumbuizaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani, Sean "Diddy" Combs ndiye anayeongoza.
Ufanisi wake unatokana na ziara yake ya majuzi Marekani, mkataba wa mauzo kati yake na kampuni ya vodka na hatua yake ya kuuza nembo yake ya mavazi ya Sean John.
Beyonce na JK Rowling wanashikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, lakini jambo la kushangaza ni kuwa wanawake katika orodha hiyo ya wasanii na wachezaji 100 ni asilimia 16 pekee.
Wanamuziki watano wa Hip Hop matajiri zaidi duniani
Walioingia katika orodha hiyo mara ya kwanza mwaka huu ni pamoja na Kylie Jenner, aliye nafasi ya 59.
Yeye ndiye wa umri mdogo zaidi katika orodha hiyo, akiwa na miaka 19.
Mapato yake yanatokana sana na kipindi cha uigizaji wa maisha ya uhalisi runingani cha familia yake, kipindi cha Keeping Up with the Kardashians. Alipokea mapato pia kutoka kwa kampuni ya manukato na vipodozi ambayo ina jina lake, nembo ya mavazi na pia kushirikishwa katika kutangaza na kuuza bidhaa mbalimbali.
Nusu ya walio katika 10 bora ni wanamuziki, lakini kuna wachezaji wawili - Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James.
Hii hapa orodha ya 10 bora:
1. Sean "Diddy" Combs - $130m (£102m)
![]() |
| Combs alijipatia jumla ya $70m baada ya kuuza theluthi ya biashara yake ya mavazi.( Reuters) |
2. Beyonce Knowles - $105m (£82.7m)
![]() |
| Nyota huyu kwa sasa ana mimba ya pacha. (Reuters) |
3. JK Rowling - $95m (£74.8m)
![]() |
| Rowling majuzi amemaliza kuandika hadithi ya filamu ijayo ya Fantastic Beasts. (Reuters) |
![]() |
| Mwanamuziki huyu kutoka Canadian alijishindia tuzo kadha mwezi jana.(AFP) |
5. Cristiano Ronaldo - $93m (£73.2m)
6. The Weeknd - $92m (£72.45m)
![]() |
Albamu yake ya karibuni zaidi, Starboy, iliibuka ya tatu kwa mauzo wiki ya kwanza Marekani mwaka 2016.
Majuzi alishirikiana na Lana Del Ray katika wimbo Lust for Life.
7. Howard Stern - $90m (£70.86m)
![]() |
Jaji huyu wa zamani wa America's Got Talent kwa sasa ana mkataba wa miaka mitano na Sirius XM Radio.
8. Coldplay - $88m (£69.33m)
Coldplay majuzi aliigiza katika tamasha la One Love Manchester.( Reuters)Coldplay wamerejea kwenye orodha hii baada ya kufanikiwa kwa ziara yao ya kimuziki waliyoipatia jina Head Full of Dreams, ambayo ilimalizikia Australia na New ZealandDesemba. Ni habari njema kwa wanaotoa msaada wka hisani, kwani bendi hiyo hutoa asilimia 10 ya faida yao kwa hisani.
9. James Patterson - $87m (£68.53m)
Kuna mwandishi mwingine orodha hii - Patterson ambaye amechapisha vitabu zaidi ya 130 na anaaminika kuwa mwandishi vitabu aliyeuza vitabu vingi zaidi ambaye bado yuko hai.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton kwa sasa anaandika kitabu kuhusu White House kwa ushirikiano naye.
10. LeBron James - $86m (£67.8m)
Hilo lilimfanya kuwa mchezaji wa tatu pekee wa NBA kulipwa $30m msimu mmoja baada ya Michael Jordan na Kobe Bryant.
Pia, hushirikishwa kuudha bidhaa za kampuni kama vile Nike, Coca-Cola na Beats ya Dre. (BBC)











No comments