Dennis Rodman, Mmarekani rafiki wa Kim Jong-un arudi tena Korea Kaskazini

Rais
wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un (kushoto) akiwa na 'rafiki yake wa
maisha', Dennis Rodman (kulia) ambaye ni mcheza kikapu wa zamani wa
Marekani.
BEIJING, China
MCHEZAJI wa zamani wa mpira wa kikapu, Dennis
Rodman amerejea Korea Kaskazini katika kile kinachoelezwa kuwa kumsalimia ‘rafiki
yake wa maisha’ na kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-un.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege mjini hapa, Rodman alisema kuwa ‘anajaribu
kuungua njia’ ya kueneza mchezo wa kikapu nchini humo.
“Ninajaribu
kufungua njia na ndiyo maana ninaelekea nchini humo,” alisema nyota huyo wa
kikapu ambaye alianzisha urafiki na Kim Jong-un mwaka 2013 baada ya safari yake
ya kwanza nchini humo.
Kwa upande
wao, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani, ilieleza kwamba wanafahamu juu ya
safari ya nyota huyo na kuongeza kwamba anasafiri kama raia wa kawaida na
kumtakia heri na fanaka kwenye safari yake.
“Tunafahamu
kuhusu safari ya Rodman (Dennis) na anasafiri kama raia yeyote wa kawaida
lakini tumewaonya Wamarekani kuhusu kusafiri kwenda Korea Kaskazini. Hilo ni
kwa usalama wao,” alisema Thomas Shannon ambaye ni ofisa wa juu kwenye wizara
hiyo.
No comments