Yahya Jammeh aliiba dola milioni 50 kutoka kwa serikali
![]() |
| Jammeh alikimbia kuenda nchini Equitorial Guinea baada ya miaka 22 uongozini. (Picha AFP) |
Kwa sasa mahakama imeagiza kutwaliwa kwa mali yake yote yaliyosalia nchini Gambia.
Jammeh alikimbia kuenda nchini Equitorial Guinea baada ya miaka 22 uongozini.
![]() |
| Watu wa Gambia wanataka haki baada ya miaka 22 ya utawala wa Jamme. (Picha AFP) |
Magari ya kifahari na bidhaa zingine ziliripotiwa kuingiza kwenye ndege ya mizgo ya Chad wakati Jammeh alikuwa akiondoka nchini humo.
Pesa hizo zilitajwa kuwa dola milioni 11 na waziri wa masuala ya ndani Mai Ahmad Fatty, ambaye wakati huo alikuwa msaidizi wa rais Adama Barrow.
Lakini siku ya Jumatatu waziri wa sheria Abubacarr Tambadou, alisema kuwa bwana Jammeh aliiba dola milioni 50 kati ya mwaka 2006 na 2016.


No comments