Header Ads

ad

Breaking News

MWAMBUSI:MECHI YA TOTO AFRICANS ITAKUWA NGUMU KWETU

Kocha-Mwambusi
Kocha msaidizi wa Yanga SC, Juma Mwambusi  ameizungumzia mechi yao ya kesho dhidi ya Toto Africa kama mechi ngumu na yenye ushindani mkubwa kutokana hali waliyonayo wapinzani wao.

Mwambusi ametanabaisha wao kama benchi la ufundi wameiandaa vyema timu yao kucheza kwa ushindani ili washinde mechi hiyo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kubeba ubingwa wa ligi kuu.
Angalizo kwao ni ushindani dhidi ya Toto Africa ambao wanahitaji alama tatu ili wasishuke daraja na uchovu ( fatigue ) wa wachezaji wao kwa kucheza mechi mfululizo.
” tunatambua Toto kesho watacheza kwa tahadhari kubwa ili kupata ushindi lakini tumewaandaa vyema wachezaji kimbinu, kiufundi na kisaikolojia ili kushinda uchovu na kucheza kwa moyo wote ” alieleza kocha huyo.
Mwambusi alikwenda mbali zaidi kwa kusema anafahamu Toto Africa watakuja kwa mchezo wa kukamia hata kuwashangaza wengi kwanini wanapambana sasa wasishuke daraja lakini wao kama Yanga SC wanalifahamu hilo na wanazoefu nalo kama ilivyokuwa katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Mbeya City.
” tunafahamu watakuja kwa kukamia dhidi yetu na tumejiandaa vyema kiufundi kwa hilo . Kushinda mchezo wa kesho ni muhimu sana kwetu kuelekea ubingwa hivyo tahadhari zote tumechukua ” alisema Mwambusi.
Yanga SC watacheza na Toto Africa kesho uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mechi yao ya 29 kuelekea mwishoni mwa msimu na alama zao 65 kileleni mwa ligi .

No comments