MABALOZI WA VIJANA WA EAC WATOA SOMO KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA STELLA MARIS, MTWARA
Mwandishi Wetu
Mabalozi
wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel wamekutana na
Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, kwa lengo la
kutoa mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini
kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika
Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017.
Jumla ya Wanafunzi 230 walihudhulia Warsha hiyo.

Mabalozi
wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel (wa tatu
na nne kushoto) wakiwa wameshika Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
pamoja na baadhi ya Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani
Mtwara, wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa
Chuo, Mei 12, 2017.

Naibu
Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel
(aliyesimama) akiwasilisha mada katika
Warsha ya siku moja kwa Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo
Mkoani Mtwara, juu ya umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki
na kuuimarisha Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, iliyofanyika katika
Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017.

Wanafunzi
wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, wakimsikiliza kwa
makini Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo
Mayenga.

Sehemu ya wanafunzi hao wakiwa kwenye Warsha hiyo.

No comments