BAADA YA KUTOLEWA AFCON, KWA MUJIBU WA TFF HIKI NDICHO WATAKACHOFANYA SERENGETI
![]()  | 
| Kikosi cha Serengeti Boys | 
Safari ya Serengeti Boys - timu ya 
Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17, inaendelea licha ya jana Mei 
21, mwaka huu kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya kuwania taji la 
Afrika hapa Port Gentil nchini Gabon.
Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na 
Niger katika mchezo uliofanyika , hivyo kufanya matokeo ya timu zote 
mbili kufanana kwa pointi, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tangu 
kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15, mwaka huu.
Serengeti Boys ilikuwa Kundi B pamoja na
 Mali iliyoongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi saba, ikifuatiwa na 
Niger yenye pointi nne sawa na Tanzania pamoja na Angola iliyoambulia 
pointi moja.
Licha ya Serengeti Boys kulingana na 
Niger, lakini wapinzani wa Tanzania walipenya kwenda hatua ya nusu 
fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa faida ya ushindi katika mchezo
 ambao umekutanisha timu hizo.
Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF 
inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana timu 
mbili zenye uwiano wa pointi na magoli kinachoangaliwa hapo ni timu gani
 ilimfunga mwenzake walipokutana na ndipo matokeao hujulikana,
Kwa jana Mei 21, mwaka huu hali hiyo 
ilijitokeza hivyo Niger kusonga mbele kwa kuwa aliifunga Tanzania bao 
1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Prt Gentil nchini Gabon.
Akizungumzia matokeo hayo, Rais wa 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema: 
“Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.”
Alizungumza hayo kwa nyakati tofauti, 
Malinzi alisema: “Tujipange sasa kwa yafuatayo: Michezo ya kufuzu 
(Qualifiers za 2019 Afcon U20  zinafanyika mwakani kuanzia mwezi June. 
Vijana hawa watashiriki.
“AFCON U17 finals (Fainali za AFCON za 
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17) zinafanyika Tanzania mwaka 
2019,” amesema Malinzi na kuongeza: “Serengeti Boys hii ya sasa inakuwa 
Ngorongoro Heroes (Vijana wa u20 na ikishapumzika kwa muda, itaingia 
tena kambini.”
Amesema kwamba vijana wa Tazania wenye 
umri wa chini ya miaka 15, walioko Shule za Alliance Mwanza wanakuwa 
Serengeti Boys wapya.
“Hakuna muda wa kusononeka ni kuchapa 
kazi tu. Kikubwa tunaandaa Taifa stars ya kwenda World cup 2026 na 
qualifiers zake zitaanza mwaka 2024. Kwa sasa timu inajiandaa kuingia 
kambini kwa ajili ya kuivaa Lesotho,” amesema.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari 
Shime amesema timu yake imepoteza mchezo huo kwa makosa ya kimchezo na 
bahati haikuangiwa kwa vijana wa Tanzania katika mchezo dhidi ya Niger. (kwa hisani ya www.salehjembe.blogspot.com)

No comments