YANGA YAANZA NA MOTO LIGI KUU, YAITANDIKA 3-0 AFRICAN LYON
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABINGWA
watetezi, Yanga SC wameanza vizuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Pongezi
kwa wafungaji wa mabao hayo, viungo Deus David Kaseke aliyefungua
biashara nzuri kipindi cha kwanza, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Rajab Mrope wa Ruvuma, Mirambo
Tshikungu wa Mbeya na Janeth Balama wa Iringa, hadi mapumziko Yanga
walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Kaseke dakika ya 18, akimalizia pasi ya winga Simon Msuva, ambaye leo alikuwa katika kiwango chake.
Mfungaji wa bao la kwanza la Yanga, Deus Kaseke akifurahia kwa ishara kwenye kibendera leo. Kushoto ni Donald Ngoma
Baada
ya bao hilo, Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi, lakini Lyon
iliyokuwa ikiwategeshea mitego ya kuotea wapinzani wao, haikuweza
kuruhusu bao lingine.
Kipindi
cha pili, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der
Pluijm ilirejea vizuri zaidi na kufanikiwa kutawala zaidi mchezo.
Haikuwa ajabu mabingwa hao watetezi walipopata mabao mawili zaidi kipindi hicho na kuamsha shangwe zaidi za mashabiki wake.
Simon
Msuva alifunga bao la pili dakika ya 60 akimlamba chenga kipa Mcameroon
Youthe Rostand baada ya pasi ya Mzimbabwe Thabani Kamusoko kabla ya
Juma Mahadhi kufunga la tatu dakika ya 90, akimalizia pasi ya kinda
Yussuf Mhilu.
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa African Lyon, Hamad Tajiri
Kiungo Deus Kaseke akimtoka beki wa Lyon, William Otong
Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe akifumua shuti katikati ya wachezaji wa African Lyon
Beki wa Yanga, Hassan Kessy (kushoto) akipoga krosi pembeni ya wachezaji wa Lyon
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa African Lyon, Hamad Tajiri




Winga wa Yanga, Simon Msuva akimtok beki wa Lyon, Amani Peter
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, bao pekee la beki Haruna Shamte limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya timu yake ya zamani, Toto African Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, bao pekee la beki Haruna Shamte limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya timu yake ya zamani, Toto African Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kikosi
cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji,
Andrew Vincent, Vincent Bossou, Simon Msuva/Juma Mahadhi dk76, Thabani
Kamusoko, Donald Ngoma/Matheo SImon dk88, Amissi Tambwe na Deus
Kaseke/Yussuf Mhilu dk89.
African
Lyon; Youthe Rostand, Baraka Jaffar, Halfan Twenye, Hamad Tajiri,
William Otong, Omar Salum, Amani Peter/Awadh Juma dk46, Mussa
Nampaka/Abdul Hilal dk74, Omary Abdallah/Ramadhani Kipalamoto dk74, Hood
Mayanja na Tito Okello.
No comments