SIMBA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA JKT RUVU UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI

KOCHA msaidizi wa Simba Jackson
Mayanja amesema kuwa kikosi chake kilicheza vizuri sema mapungufu katika
safu ya ushambuliaji yameinyima ushindi timu yake.
Simba imelazimishwa suluhu ya kutokufungana na JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja amesema kuwa bado wanajipanga kuweza kuhakikisha wanashinda kwenye michezo yao inayofuata.
Katika mchezo wa awali Simba walitoka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Ndanda na baada ya matokeo haya wanasalia na alama nne huku kwenye michezo mingine Azam amefanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea mchezo ulipigwa uwanja wa Chamazi.
Mtibwa Sugar nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ndanda huku Mwadui Fc wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.

No comments