UKAWA KUWANUFAISHA WAKULIMA WA KOROSHO NA UFUTA MIKOA YA KUSINI
Mgombea
Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwasili katika jimbo
la Mtama katika mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Lindi ambapo
katika hoyuba yake aliwaambia wananchi wa mkoa wa Lindi kuwa endapo
serikali ya Ukawa itaingia madarakani itaboresha bei ya ufuta na korosho
ili kuwanufaisha wakulima wa zao hilo. (Picha na Francis Dande)
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Habib Mnyaa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Mbunge wa Lindi mjini akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Tunausapoti Ukawa.....
Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Guninita akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Mgombea
Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimiana na mfuasi
wa Ukawa wakati alipowasili katika mkutano wa kampeni katika jimbo la
Mtama mkoani Lindi.
Wafuasi wa Ukawa wakishangilia.
MAGUFULI AFUNGA KAZI MKOANI MTWARA,AHIDI KUSHUSHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara
waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni
unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa.
Dkt
John Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi
mkuu mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa
bati na saruji,amesema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya
watanzania wote na hivyo atapunguza bei ya saruji na bati na hilo
litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo.
"Serikali
ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya
mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na
saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo
lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.
Alisema
anatambua kiu ya watanzania ni kutaka mabadiliko ya maendeleo na kwamba
Serikali yake itasimamia kuleta maendeleo ya wananchi na kazi hiyo
anaiweza na ndio maana anaomba urais. " Ndugu zangu watanzania serikali
ya Magufuli inakuja kuendelea pale ambapo awamu nyingine
zimeishia.Tumetoka mbali ,tupo mbali na tunakwenda mbali.Nataka tuwe na
maendeleo makubwa na hilo serikali yangu ndio kazi itakayofanya,"alisema
Dk.Magufuli huku wananchu wakimshangilia kwa mayowe.
Dk Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo akishinda uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile Eimu ya bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50 kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo

Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara
waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni
unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa.
Dk
Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6
ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo aakishinda
uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile ile ya bure kutoka darasa
la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba
Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50
kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na
biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo
Wakazi
wa mji wa Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni za CCM,unaofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa
CCM,wakimsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.
Dk
Magufuli akizungumza na mtoto Riziki Faraji na pia alimpa kiasi
kadhaa cha fedha kwa ajili ya kununulia sare ya shule alipomuona wakati
msafara wake ulipozuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kitama A, mkoani
Mtwara
Dk
Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia
katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziwani Mtwara
Vijijini
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Mtwara mjini,Murji Hasnein Mohamed akiwasalimia
maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara waliofurika kwenye uwanja wa
Mashujaa katika mkutano wa kampeni za CCM,jioni ya leo ambapo Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli aliwahutubia wananchi hao .
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na
wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani
Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa
wingi.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja
na wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani
Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa
wingi.
No comments