DR. JOHN POMBE MAGUFULI ALITIKISA JIJI LA TANGA, WANANCHI WAFURIKA VIWANJA VYA TANGAMANO KUMSIKILIZA

Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja
vya Tangamano mjini Tanga leo, Dr. Magufuli amewaomba wananchi wa Tanga
kumpigia kura za ndiyo ili aweze kufanya kazi na kulitumikia taifa,
yeye kwake ni Kazi tu! kwani hata biblia inasema “Asiyefanya kazi na
asile”.
Ameongeza kwamba mara
atakapochaguliwa na kuongoza nchi ya Tanzania atahakikisha anafufua
viwanda mbalimbali vilivyopo nchini na kujenga viwanda vipya
vidogovidogo, vya kati na vikubwa ili kupunguza tatizo la ajira nchini
lakini pia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla wake, Huku akiahidi kubana
matumizi hovyo ya fedha za serikali ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa
hali ya chini ambao wanasumbuka na umasiki.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Mwezi Oktoba Mwaka huu nchini
kote ukishirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-TANGA)
Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
zake uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga.
Mwanamuziki nguli hapa nchini Diamond Platnumz akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano huo wa kampeni.
Mwanamuziki Ali Kiba akionyesha uwezo wake katika jukwaa wakati akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Tanga.
Mzee Yusuf Makamba akizungumza
neno katika mkutano huo na kuwafunda wananchi wa mkoa huo kutopoteza
kura yao na kumpa Dr. John Pombe Magufuli wa CCM ili awatumikie.
Tangamano ikiwa imetapika umati wa wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli.
Yamoto Band wakitifua jukwaa.
Mwanamuziki wa muziki wa taarab Mzee Yusuf naye akipagawisha wananchi katika mkutano huo.
Kada wa CCM na mwenyekiti wa
Chama cha walemavu Ndugu Amon Mpanju akiwahutubia wananchi na kumpigia
debe Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
Ummy Mwalimu akizunguza jambo katika mkutano huo.
Mwigulu Nchemba mgombea ubunge
jimbo la Iramba Magharibi naye akatema cheche na kusema wapinzani ni
watu wa dili tu, kila kitu dili.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli
akimkaribisha Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli mkoani Tanga.

Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akiwapungia mikono wananchi wa mkoa wa Tanga mara baada ya
mkutano kumalizika.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza na mgombea ubunge wa jimbo la
Bumbuli Mh. Januari Makamba kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo la Iramba
Magharibi Mwigulu Nchemba.


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Pangani
leo.

Baadhi ya vijana waliokuja
kumsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakifuatilia hotuba yake
huku wakiwa juu ya miti.
Akina mama wakiwa wamejifunika na
mabango yenye ujumbe wa kampeni ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli
yanayosema “Magufuli Hapa Kazi Tu” wakiwa katika mkutano wa kampeni
mjini Pangani.

Vijana wakiwa katika miti
wakimsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia
wananchi.

Hapa ni rangi za CCM tu.

Hii nyumba iliyopo kijiji cha
Mkuza Mheza ni full mchanganyiko wao hawana bifu wanadhihirisha kwamba
siasa siyo uadui kwa kuweka picha za wagombea wa CCM na UKAWA.

Mzee huyu na Mgombea Udiwani wake kata ya Mkuza.

Hawa wanaonekana wamekunwa na
sera za Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli

Hapa wakapaza zaidi sauti zao wakisema “Wewe ni Tingatinga letuuu!!

Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akimnadi Balozi Adadi Rajabu ambaye anagombea ubunge kupitia
jimbo la Muheza.

Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni mjini Muheza.

Dr. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi Adadi Rajabu mgombea ubunge wa jimbo la Muheza.

Mchezea Chatu wa ngoma za utamaduni naye hakusita kufanya mambo yake katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Muheza.

Vijana wa Kabuku wakampokea Dr. John Pombe Magufuli.

Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata akiwa njiani kwenda Muheza,
Pangani na Tanga mjini kwa ajili ya mikutano ya Kampeni ambapo
aliwaambia atahakikisha anatatua tatizo la maji Mkata mara
atakapochaguliwakuongoza nchi ya Tanzania.

Wananchi wakimsikiliza Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM
Dr. John Pombe Magufuli huku kukiwa na madumu kwa ajili ya kuchotea
maji Mkata ina tatizo kubwa la maji safi ya kunywa.
No comments