Bayport yazindua huduma mpya ya Jibayportphonishe
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
kushoto, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya
simu za mikononi aina ya Huawei ijulikanayo kama 'Jibayportphonishe',
uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Micka Mavoa,
Mkurugenzi wa Cape View, Kampuni inayoshirikiana na Bayport katika
huduma hiyo ambayo mteja akikopa simu atapelekewa hadi mahala
anapohitaji ifike. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial
Services, imezindua huduma yake mpya ya kukopesha (Smartphone) simu za
mikononi aina ya Huawei zenye thamani ya Sh 140,000, ikiwa na lengo la
kuwawezesha Watanzania ambao ni watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni binafsi zilizoidhinishwa kumiliki simu wakati wowote ili
ziwakwamuwe katika suala zima la mawasiliano ya simu za mikononi, huduma
inayotambulika kama 'Jibayportphonishe'.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo ya mikopo ya simu za mikononi kumekuja siku chache
baada ya taasisi hiyo pia kuzindua huduma ya bima ya magari, pikipiki na
bajaj, ambapo zote kwa pamoja ni mkombozi kwa Watanzania, wakiwamo wale
wenye kipato cha chini na cha kati.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Masoko na Mawasiliano wa
Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa
huduma hiyo kutaifanya jamii iwe katika kiwango kizuri cha mawasiliano,
hivyo kukuza pia uchumi wao.
Mkurugenzi wa Cape View, Micka Mavoa, kulia akizungumza jambo.
Alisema
kwamba badala ya mtumishi wa umma na wale wa kampuni binafsi
zilizoidhinishwa kuwekeza kidogo kidogo ili wanunuwe simu watakazo, sasa
wanaweza kukopeshwa simu hizo na kupelekewa hadi katika maeneo yao
wanayopatikana. Alisema simu hizo zitaambatana na ofa ya intaneti MB 500
bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka katika Kampuni ya Simu za
Mikononi ya Vodacom Tanzania, huku mteja akilazimika kulipa Sh 9000 kila
mwezi, katika kipindi cha miezi 24.
No comments