Header Ads

ad

Breaking News

Ndege nyingine yapotea nchini Indonesia



papu
Indonesia imeingia kwenye rekodi mbaya ya ajali za ndege, wakati tayari ajali mbili  zimeripotiwa ndani ya mwaka mmoja uliopita, ikiwemo Indonesia Air iliyoanguka katika bahari ya Java ikitoka Sura Baya kuelekea Singapore na kuua watu wote 192.
Taarifa hizo zimerudia tena nchini humo baada ya ndege moja iliyobeba abiria 54 kupoteza mawasiliano na idara ya kituo cha udhibiti wa safari za ndege.
Maaofisa wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa, ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Trigana Air ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil Mashariki mwa jimbo la Papua kabla ya kutoweka.

Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa, hatua za kuisaka ndege hiyo zimeanza na zinashirikisha mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri utafutaji wa ndege hiyo.

No comments