DR. MAGUFULI AITIKISA SONGEA, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa
majimaji mjini Songea leo ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya
wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo
wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa
anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya
chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa
kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Amesema pia serikali yake
itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza
mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi ,
wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Amesema ataongeza zaidi kasi
yake katika utendaji tofauti na alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo
awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa akichaguliwa na watanzania
kuwa rais yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua
asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia
alitembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kada maarufu wa
CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki miezi kadhaa
iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na
kuzikwa nyumba ni kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma(PICHA
NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SONGEA)

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima
katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika
kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya
CCM Ndugu William Lukuvi.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada
la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani
Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akishuka
kutoka katika kivuko cha Mv Lituhi mara baada ya kuvuka mto Luhuhu
akitokea mkoani Njombe wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma
kuendelea na kampeni zake.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipunga mkono
mara baada ya kuvuka mto Luhuhu akielekea Mbinga mkoani Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi.
Umati wa wananchi ukiwa umefurika
katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika mkutano wa kampeni
uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli.
Mmoja wa wana CCM akifuta vumbi
kwenye picha ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi mjini Mbinga kwenye uwanja wa Taifa kumsikiliza Dr John Pombe Magufuli.
Kada wa CCM Bw. Amon Mpanju akiwahutubia wakazi wa mjini Songea mkoani Ruvuma leo.
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita.
Mabasi Maalum ya Kampeni za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea wa CCM jimbo la Songa Mjini Mh. Leonidas Gama.
Baadhi ya wana CCM wa wilayani
Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa
CCM kwenye uwanja wa Taifa uliofanyika katika mji huo.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
mjini Mbinga.
Baadhi ya wananchi wakiwa
wameshika picha za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza
mgombea ubunge wa jimbo la Mbinga Komredi Sixtus Mapunda wakati
alipokuwa akiwaomba kura wananchi wa mji wa Mbinga.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi Mh.
Jenista Mhagama mgombea ubunge wa jimbo la Peramiho katika mkutano
uliofanyika Peramiho.
Wana Peramiho wakimkaribisha Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Peramiho ikizizima kwa bendra za CCM wakati wa mapokezi hayo.
Umati uliohudhuria katika mkutano huo
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia
katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mkutano wake
uliofanyika Peramiho.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi
Ilani ya Uchaguzi Mh.Jenista Mhagama ambaye Mgombea ubunge wa jimbo la
Peramiho
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa na
watoto mara baada ya kumaliza mkutano wake Peramiho.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.
Majimaji ikiwa imetapika
Kundi la TOT likifanya vitu vyake jukwaani.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na viongozi
mbalimbali wakiwa wameketi meza kuu.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Songea mjini Dr. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi na kumpigia
debeMgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk.
John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja
wa Majimaji mjini Songea.
Huyu naye alivaa makufuli
kichwani na shingoni kupeleka ujumbe wa mapenzi yake kwa Mgombea wa
Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli.
Kutoka kulia ni Mwingulu Nchema, Jenista Mhagama na William Lukuvi wakiteta jambo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Songea mjini Mh. Leonidas gama akijinadi kwa wananchi kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji.
No comments