Gor Mahia yatangulia robo fainali Kombe la Kagame
Gor Mahia wana uhakika wa kutinga robo
fainali ya michuano ya Kagame baada ya ushindi wao wa pili leo dhidi ya timu za
Tanzania.
Jumamosi wakati wa ufunguzi, waliifunga
Yanga mabao 2-1, leo wamerudi tena kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
na kuitandika KMKM kwa mabao 3-1.
Wakati Gor Mahia walikuwa wa kwanza kupata
bao kupitia kwa Myarwanda Meddy Kagere, KMKM walisawazisha mfungaji akiwa Anthony Simon.
Olunga alifunga bao la pili katika dakika ya 70, kabla ya kupiga la tatu katika dakika ya 82 na kuihakikishia Gor ushindi huo wa pili mfululizo dhidi ya timu za Tanzania.
No comments