Balozi Seif Idd afungua Tamasha la 18 la Filamu la nchi za Jahazi
Meneja
wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika
ukanda wa Afrika Mashariki (ZUKU), Maud Roger akiahidi taasisi
yake kuendelea kusaidia vipaji vya vijana katika utengenezaji wa filam
zilizo bora Nchini.
Mkurugenzi
wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF), Profesa Martin
Mhando akitoa neneo la makaribisho kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo hapo
shangani. Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF), hapo Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF), hapo Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akiwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, akijumuika pamoja na baadhi ya viongozi kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar hapo Double Tree By Hilton Shangani mjini Zanzibar leo. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mhmoud Thabit Kombo na msanii wa filam ya sarafina kutoka Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF), Mahmoud Thabit Kombo akitoa neon la kumkaribisha mgeni rasmi kulizindua Tamasha hilo hapo Double Tree By Hilton Shangani.
Msanii
Mkongwe wa nyimbo kutoka Johannesburg Nchini Afrika Kusini Doroth
Masuka akipongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali pamoja na
washirika wake katika kuimarisha vipaji vya wasanii hapa Nchini.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na washirika
wa Tamasha la Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya
kulizindua Tamasha hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed
Shein. Kulia kwa
Balozi Seif Idd ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michiezo Mh,
Said Ali Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia, kukuza
vipaji vya wasanii katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ZUKU) Bibi Maud
Roger. Kushoto
kwa Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za
Jahazi Zanzibar (ZIFF) Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Msanii Maarufu
Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka nchini
Afrika Kusini, Bibi Laleta Kumalo.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na washirika
wa Tamasha la Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya
kulizindua Tamasha hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed
Shein. Kulia kwa
Balozi Seif Idd ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michiezo Mh,
Said Ali Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia, kukuza
vipaji vya wasanii katika Ukanda wa Afrika Mashariki (ZUKU) Bibi Maud
Roger. Kushoto
kwa Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za
Jahazi Zanzibar (ZIFF) Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Msanii Maarufu
Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka nchini
Afrika Kusini, Bibi Laleta Kumalo. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono juhudi
zinazochukuliwa na Uongizi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za
Jahazi Zanzibar { ZIFF } katika azma yake ya kuijengea nguvu tasnia ya
Filam Nchini inayoonekana kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya
Utalii.
Kauli
hiyo imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati
akilizindua Tamasha la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi
Zanzibar { ZIFF } hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Double
Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Dr.
Shein alisema kwamba Tamasha la Nchi za jahazi limekuwa na mchango
mkubwa katika kuitangaza Zanzibar Kimataifa hali ambayo imetoa ushawishi
kwa wageni na watalii wengi kuamua kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar
kujionea mazingira na rasilmali zilizopo.
Alisema
kupitia Tasnia ya filam zinazotayarishwa na wasanii mbali mbali kwa
kushirikiana na wadau wa Fani hiyo chini ya Wataalamu wa Ziff wageni na
watalii mbali mbali Duniani wamekuwa wakivutiwa na fukwe pamoja na
Utamaduni uliojaa ukarimu wa Watu wa Visiwa vya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi
za Jahazi Zanzibar { ZIFF } kuendelea kufanya juhudi zaidi za
kuwashawishi wasanii wa Kimataifa kuzitumia Fukwe na Tamaduni za
Zanzibar katika kutengeneza Filam mbali mbali kwa lengo la kuitangaza
zaidi Zanzibar Kimataifa.
“
Zanzibar ni Visiwa vya maumbile ya Utamaduni ya Ukarimu pamoja na
fukwe za kuvutia mambo ambayo yakitangazwa vyema wasanii wa Kimataifa
wanaweza kushawishika kuyatumia katika kutengeneza Filamu zao “.
Alifafanua Dr. Shein.
Alifahamisha
kwamba Tamasha la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi, Tamasha la
Iddi, Tamasha la Mzanzibari pamoja na Sherehe za Mwaka Kogwa
zinazofanyika Makunduchi ni Mambo muhimu yanayopaswa kuimarishwa katika
kukuza na kusimamia Utamaduni na Historia ya Zanzibar na Watu wake.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewapongeza Wasanii
wa Maigizo pamoja na Filam Nchini kutokana na kazi kubwa wanayoendelea
kuifanya ya kuelimisha Jamii sambamba na kuwapatia Burdani.
Alisema
mbali ya Tasnia hiyo kutoa ajira pana kwa kundi kubwa hasa Vijana
Nchini lakini pia imepanua soko la filam za nyumbani na kuleta unafuu
kwa kila mtu kumudu kununua na kuangalia kazi za wasanii wa hapa Nchini
hali iliyopelekea kufikia asilimi 80% ya filamu za Kiswahili
zinazoangaliwa tofauti na miaka iliyopita nyuma.
Mapema
Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii
katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger aliahidi
kwamba Taasisi yake itaendelea kukuza vipaji vya wasanii kwa lengo la
kufikia kiwango kinachokubalika Kimataifa.
Bibi
Roger alisema hatua hiyo muhimu itaweza kuwajengea uwezo wa kiajira
badala ya kusubiri kutegemea zile za Serikali ambazo kwa sasa upo
upungufu mkubwa hata katika Mataifa yaliyoendelea.
Meneja
wa Taasisi hiyo ya Zuku alifahamisha kwamba mpango maalum umeandaliwa
na Uongozi wa Taasisi hiyo baina ya miaka sita na kumi kwa kuwadhamini
Vijana wapatao Kumi wanaopata Mafunzo ya msingi kuweza kutengeneza Filam
zitazokubalika Kimataifa.
Wakitoa
salamu zao kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam
la Nchi za Jahazi Msanii Gwiji Duniani kutoka Nchini Afrika Kusini
Laleta Kumalo aliyeigiza filam Maarufu ya sarafina pamoja na Msanii
Mkongwe wa Nchi Hiyo Doroth Masuka wameelezea faraja yao kutokana na
Serikali kupitia taasisi za kijamii zilivyojikita katika kusaidia vijana
kwenye fani ya sanaa.
Akimkaribisha
mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la 18 la Ziff Mwenyekiti wa
Bondi ya Tamasha hilo Mahmoud Thabit Kombo alisema Ziff itaendelea
kushirikiana na wadau wote wa ndani na nje ya nchi katika kuona Taasisi
hiyo muhimu inazidi kuimarika.
Mahmoud
Thabit Kombo alisema uimarikaji huo utawapa nguvu na ari Vijana
walioamua kujiajiri kupitia Tasnia ya Filam inayoonekana kupata umaarufu
siku hadi siku hapa Duniani.
Uzinduzi
wa Tamasha hilo la 18 la Kimataifa la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar
(ZIFF) limekwenda sambamba na siku yake lililoasisiwa rasmi Tarehe 18
Julai Mwaka 1997 likitimiza umri wa miaka 18 sasa.
No comments