Header Ads

ad

Breaking News

Azam FC yaanza vema Kombe la Kagame

 Azam FC imeanza michuano ya Kagame kwa kuichapa timu ngumu ya KCC kwa bao 1-0.
 

Shujaa wa Azam FC leo ni nahodha wake, John Bocco aliyefunga bao hilo pekee kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Licha ya ushindi huo, Azam FC walilazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na uimara wa kikosi cha Waganda hao.

Hata hivyo Shomari Kapombe, Kipre Tchetche, Bocco na Frank Domayo walionekana kuwasumbua zaidi Waganda hao.

No comments