Header Ads

ad

Breaking News

Miss Universe akiri mashindamo yalikuwa magumu

Betty Omara
Na Mwandishi Wetu

MISS Universe Tanzania, Betty Omara amerejea nchini kutoka Urusi alipokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa na kukiri kuwa, yalikuwa magumu, pamoja na kupata uzoefu mkubwa.

Betty ambaye aling’ara katika vazi la taifa kwa kuvaa vazi la mkeka lililobuniwa na mbunifu chipukizi, Mwanakombo Salim kwa kusaidiana na wasanii wa Tingatinga, alisema pamoja na kutofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, anachojivunia ni kuitangaza nchi kupitia vivutio vya utalii akiwa balozi wa Hifadhi ya Taifa (Tanapa), ambao walikuwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Universe Tanzania.

Wabunifu wengine waliomvalisha mrembo huyo ni Mama Schwari, Kiki Zimba (Kiki’s), Kali Elegance na Nasreen Kareem kupitia duka lake la Anjipai ambalo lilimpa nakshi ikiwemo mikufu na hereni mbalimbali katika kukamilishia mavazi yake na kuonekana kiafrika zaidi.

Alisema kuwa mbali ya hayo, alikuwa mrembo pekee kutoka bara la Afrika aliyechaguliwa miongoni mwa warembo nane kote ulimwenguni kushiriki katika kipindi maarufu mjini Moscow kinachooneshwa duniani kote kijulikanacho kama “Let Them Talk” kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu Andrey Malakhov.

Betty alisema kuwa, katika kipindi hicho ambacho kinapatikana kwenye mtandao, alionekana kuwafurahisha sana hadhara ya warusi katika studio na kusifiwa kwa kuwa mrembo wa kipekee na mwonekano wake wa kiafrika.

Alifafanua kuwa, baadhi ya majaji wa mashindano ya Miss Universe walikuwepo na walieleza kuvutiwa sana na Betty na kumwona kama mrembo ambaye alikuwa mwenye nafasi kubwa ya kuingia 16 bora.

“Kipindi chote nilipokuwa Urusi, nilikubalika sana na warusi wenyewe, hata vyombo vya habari vya kimataifa. Nina furaha kubwa sana kwani kilichonileta nimekifanikisha, lengo langu kubwa zaidi ya ushindi lilikuwa ni kuhakikisha naitangaza vyema Tanzania na vivutio vyake, kama vile hifadhi za taifa za Ruaha, Udzungwa, Katavi na mengineyo,” alisema Betty.

Alisema kuwa, kwa msaada mkubwa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, alifanikiwa kufanya mahojiano na gazeti maarufu la utalii nchini humo lijulikanalo jarida la utalii nchini Urusi linaliloitwa “Hot Line travel Magazine.”

No comments