John
Bayo, Mkurugenzi wa Mbio za Kilimanjaro Marathon alisema katika taarifa yake
jana kwamba wanariadha maarufu Watanzania ambao wameshiriki na kushinda
mashindano mbalimbali duniani ikiwemo Kilimanjaro Marathon watashiriki katika
mbio hizo kubwa zaidi hapa Tanzania. Baadhi yao ni pamoja na Patrick Nyangero,
Andrea Silvini, Fabian Joseph, Sarah Ramadhan, Mary Naali na Banualie Brighton.
Orodha
kamili
Full
Marathon Wanaume: Mashaka Masumbuko, Patrick Nyangero, Getuli Bayo, Faustine
Musa, Andrea Silvini
Full
Marathon Wanawake: Banuelia Bryton, Fabiola William, Ceophresina Sumawe.Nusu Marathon Wanaume: Fabian Joseph, Dickson Marwa, Uwezo Lukinga, Damina Chopa, Mohammed Dulle
Nusu
Marathon Wanawake: Sarah Ramadhani, Jacqueline Sakilu, Mary Naali
Patrick
Nyangero alishika nafasi ya pili kwenye Kilimanjaro Marathon mwaka 2009 ambapo
alimaliza mbio katika muda wa 02:15:35, ameshiriki mashindano mengine
mbalimbali yakiwemo Gold Coast Marathon, Mashindano ya Dunia huko Melbourne
Australia mwaka 2005, na baadae akashinda Nagpur Marathon huko India. Andrea
Silvini alishinda Kilimanjaro Marathon mwaka 2007 na baada ya hapo akashinda
Pune Marathon mwaka 2008 na akawa mshindi wa tatu kwenye Kilimanjaro Marathon
2008 ambapo alimaliza mbio katika muda wa 02:16:22. Banuelia Brighton alishinda
kilomita 42 kwenye Kilimanjaro Marathon 2008 katika muda wa 02:48:37 na baadae
akashinda Kigali Marathon in 2009.
Wanariadha
wengine mashuhuri waliothibitisha ni pamoja na Fabian Joseph ambaye ana rekodi
ya kushinda Kilimanjaro Marathon 2010 katika muda wa 1:03:59, ambapo alivunja
rekodi ya Mtanzania mwenzake Damian Chopa aliyeshinda mbio hiyo katika muda wa
1:04.43. Damian Chopa pia alishinda Nusu Marathon huko Edmonoton Canada mwaka
2005 katika muda wa 1:01:08.
Wanariadha
wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Mary Naali, mshindi wa Vienna
Half Marathon mwaka 2010, Sarah Marja Ramadhan ambaye alimaliza km 42
Kilimanjaro Marathon 2012 katika nafasi ya 11 katika muda wa 2:51.00 ambayo ni
rekodi binafsi nzuri zaidi katika miaka mitano.
Zaidi
ya nchi 40 zinatarajiwa kushiriki huku washiriki wan je wakitarajiwa kuwa zaidi
ya 600. Washiriki wengi watatokea Afrika Kusini, Uingereza, Zimbabwe, Kenya,
New Zealand, China, Canada, Marekani, Australia, France na Italy.
Washiriki
wa mbio hizo watakuwa na uhuru wa kuchagua mbio zipi wakimbie kati ya 42 km
Marathon, 21 Half Marathon, GAPCO Disabled Half Marathon na Vodacom 5 Km Fun
Run.
“Kilimanjaro
Marathon inatambulika kimataifa ikiwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali. Mbio
hizi huvutia wanariadha wa viwango vya juu hivyo kuwapa wanariadha Watanzania
nafasi ya kujipima ipasavyo”, alisema John Addison, Mkurugenzi wa Wild
Frontiers, waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon.
"Uandikishwaji
washiriki utafanyika Arusha tarehe 28 February kwenye Hoteli ya New Arusha
Hotel na pia tareh 1 na tarehe 2 Machi kwenye hoteli ya Keys mjini Moshi.
Hakutakuwa na uandikishwaji wowote utakaofanyika siku ya mbio tarehe 3 Machi
2013. Hata hivyo wanaotaka kujiandikisha mapema wanaweza kufanya hivyo kupitia
tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com," alisema
Addison.
Mbio
hizi zinaratibiwa na Executive Solutions huku wadhamini wakuu wakiwa ni
Kilimanjaro Premium Lager. Wadhamini wengine ni GAPCO wanaodhamini Nusu
Marathon ya Walemavu na Vodacom wanaodhamini mbio za kujifurahisha za Vodacom
5km Fun Run. Wadhamini shirikishi ni pamoja na Tanga Cement, CFAO Motors, KK
Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hotel, Kilimanjaro
Water , FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu
(UNFPA).
No comments:
Post a Comment