MWANAMUZI
wa shule ya Sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya (20) ameshinda zawadi ya gari
aina ya Vitz kufuatia shindano la siku ya wapendanao (Valentine campaign)
lililomalizika Februari 14.
Mbali
ya droo ya Vitz lenye thamani ya sh Milioni 8, pia washindi mbali mbali
walipatikana katika siku ya mwisho wa shindano hilo lililofanyika kwenye ofisi
za African Media Group (AMG).
Meneja
Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Push Media Mobile Rodney Rugambo alisema kuwa
Ndonya ameibuka mshindi baada ya namba yake kuibuka ya kwanza katika shindano
hilo lililodumu kwa takribani miazi mitatu na kutumia zaidi ya sh milioni 30.
Rugambo
alisema kuwa wahsindi wengine katika droo hiyo ni Daudi Samson (22) ambaye pia
ni mwanafunzi aliyejishindia Ipad, Tabia Lihonde (44) ambaye ni nesi anayefanya
kazi Mtwara na kuibuka mshindi wa simu ya mkononi aina ya blackberry na
Emmanuel Sanga aliyeshinda home theatre.
Akizungumza
kwa baada ya ushindi huo, Ndonya alisema kuwa amefurahi sana kwani ndoto yake
ya kushinda gari imetimia.
“Nilishiriki
katika shindano kama washindani wengine, ndoto yangu ilikuwa ni kushinda,
nashukuru nimeshinda na ushindi huu ni chachu ya kuendelea kushiriki katika
mashindano mengine yajayo, ” alisema Ndonya. Mbali ya Push Media Mobile, droo
hiyo pia iliendeshwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten na Radio ya Magic
FM na kudhaminiwa na Alliance Insurance.
No comments:
Post a Comment