12/02/2013
1.
Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo kupitia Kanuni za Uchaguzi za TFF
Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na Ibara ya
14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi la kampeni za
uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi
hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi
kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.
2.
Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa.
3.
Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza
uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi
hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Deogratias
Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI
YA UCHAGUZI TFF
WASHABIKI
WAZIUNGE MKONO AZAM, SIMBA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaka washabiki wa mpira wa miguu
kujitokeza kwa wingi wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simba
zitakazocheza mechi za mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.
Nguvu
ya washabiki ni muhimu katika kuziweza timu hizo kufanya vizuri katika mechi
hizo za nyumbani dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Libolo ya
Angola.
Azam
itacheza Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katika mechi ya
Kombe la Shirikisho wakati Simba itaikabili Club Libolo kwenye mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika itakayofanyika Jumapili. Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
LYON,
YANGA KUUMANA UWANJA WA TAIFA
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inamaliza raundi ya 16
kesho (Februari 13 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji African Lyon dhidi ya
Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro inakutanisha timu
zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo kwa
pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na Salum Bausi inakamata mkia
ikiwa na pointi tisa tu.
Nayo
Toto Africans itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka
Musoma. Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
20,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Oljoro JKT.
Nahodha
wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha wa Mtibwa Sugar
ataiongoza timu yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa
Manungu ulioko Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo huo ambapo Mtibwa Sugar
katika mechi yao iliyopita walichapwa mabao 4-1 na Azam.
UCHAGUZI
FRAT UPO PALEPALE FEB 14
Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) unafanyika
Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa
wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari 12 mwaka
huu) . Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa
mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.
Wagombea
ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu
Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.
Abdallah
Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya
Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi
wanawake yupo Isabela Kapera.
Wagombea
wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment