Ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kimataifa,
ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo nyumbani, hivyo kuwa na kibarua kigumu
katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo nchini Sudan.
Washindi hao wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
walikuwa wa kwanza kulifikia lango la wapinzani wao, lakini Kipre Tchetche
alishindwa kufunga bao dakika ya 10, baada ya kupiga shuti kali lililopanguliwa
na kipa Peter Midia.
Azam wakicheza kwa kujituma, walifanikiwa kupata bao
la kwanza dakika ya 14, lililofungwa na Abdi Kassim ‘Babi’, kwa kichwa akiunganisha mpira uliotoka kwa
Hamphrey Mieno na kuujaza wavuni.
Dakika ya 21, Tchetche alipata nafasi nzuri ya
kufunga, lakini alishindwa kuitimia vizuri krosi iliyotoka kwa Babi, baada ya
shuti lake kupanguliwa na kipa wa Al Nasri.
Al Nasri wangeweza kusawazisha bao dakika ya 27, baada
ya Kon James kuwatoka mabeki wa Azam na kupiga shuti kali lililodakwa na kipa
Mwadin Ali.
Juhudi za Al Nasri zilizaa matunda dakika ya 39,
baada ya Fabian Elius kuisawazishia bao timu yake, akitumia vizuri makosa ya
mabeki wa Azam na kuujaza mpira kimiani.
Kipindi cha pili, Azam walipata nafasi nzuri ya
kufunga bao, lakini Babi alishindwa kuwainua vitini mashabiki wao dakika ya 48,
na mpira ukaondoshwa kwenye hatari na beki Joseph Odongi.
John Bocco aliyeingia kuchukua nafasi ya Babi,
alishindwa kuitumia vizuri nafasi aliyopata dakika ya 68, baada ya mpira wa
kichwa aliopiga kudakwa na kipa wa Al Nasri, Midia.
Kipre Tchetche, alifanya kazi nzuri na kuipatia timu
yake ya Azam bao la pili dakika ya 80, kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi
uliopigwa na Hamis Mcha na kujaa wavuni.
Dakika ya 84, Bocco alishindwa kuifungia timu yake
bao baada ya shuti lake kali kupanguliwa na kipa Midia, kabla ya kumrudia, lakini
shuti lake la mwisho mpira ukapaa juu ya lango la Al Nasri.
Kipre Tchetche aliwazidishia maumivu Al Nasri kwa
kufunga bao la tatu dakika ya 90, akitumia vizuri pasi ya Mcha na kuukwamisha
mpira wavuni.
Katika mechi hiyo, mashabiki wanaokaa jukwaa
linaloaminika kutumiwa na Yanga, walikuwa wakiishangilia Al Nasri, hasa baada
ya kuwaona wakiwa katika jezi zenye rangi ya njano.
Lakini, ushindi huo wa Azam, unaweza kuwa salama
tosha kwa Yanga, ambao watavaana wiki ijayo katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Azam: Mwadini Ally, Himid Mao, Malika Ndeule, David
Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Humphrey
Mieno, Brian Umony, Abdi Kassim ‘Babi’/John Bocco na Tchetche Kipre.
Al Nasr: Peter Midia, Joseph Odongi, Mskin Ammanuel,
Abdallah Sebit, Simon Amanya, Johnson
James, Abdallmelik Sebit, Ladu Manas, Kon James, Jacob Osuru, Fabian Elias.
No comments:
Post a Comment