Tuesday, February 12, 2013

Nyamlani, Manji sasa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana uchaguzi wa TFF

Dar es Salaam: Baada  ya kuketi kwa siku mbili kupitia na kusikiliza rufaa mbalimbali zilizo katwa kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF, hatimaye kamati hiyo imetoa maamuzi yake.
Kabla ya kamati ya rufaa uchaguzi ya TFF kuketi kwa siku hizo mbili, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua waombaji kumi na mbili wa uongozi kwenye nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kutokidhi matakwa ya kikatiba.
 Waombaji hao waliochujwa ni Omari Mussa Nkwarulo aliyeomba kuwania urais na Michael Richard Wambura aliyejitosa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Makamu wa Rais.
Wengine waliochujwa wakiomba kugombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Hussein Musa, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Eliud Peter Mvella, Farid Nahdi, Omari Isack Abdulkadir na Shafii Kajuna Dauda.
Kwa upande wa uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechujwa ni Christopher Peter Lunkombe aliyekuwa akiomba nafasi ya ujumbe katika Kamati ya Uendeshaji.
                           
Mwenyekiti wa kamati ya Rufaa ya TFF,  Iddi Mtiginjola
 Hata hivyo baadaye kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF ilipokea rufaa mbalimbali kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika Februari 22 na 24 mwaka huu.
Waliowasilisha rufani mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ni pamoja na waombaji uongozi saba walioenguliwa katika kinyang’anyiro hicho. Warufani hao ni Omari Mussa Nkwarulo na Michael Richard Wambura walioomba kugombea urais na umakamu wa rais.
Wengine ambao waliomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali ni Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Omari Isack Abdulkadir (Dar es Salaam), Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya) na Shaffih Kajuna Dauda (Dar es Salaam).
Warufani wengine ni wadau ambao waliweka pingamizi dhidi ya baadhi ya waombaji uongozi katika TPL Board na TFF, pingamizi ambazo zilitupwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa sababu za kiufundi.
Wadau hao waliokata rufani ni Agape Fue dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Jamal Malinzi kugombea urais, Medard Justinian dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Athuman Nyamlani kugombea urais, na Frank Mchaki dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Hamad Yahya kugombea uenyekiti wa TPL Board.
Majibu ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF chini ya mwenyekiti wa Iddi Mtingijola yaliyotolewa mbele ya waandishi wa habari usiku ni kama ifuatavyo.
Kanda ya Dar es Salaam rufaa ya Shafii Dauda imeshinda na hivyo basi jina lake limerudishwa katika kinyanyiro cha uchaguzi na kwamba maamuzi ya kamati ya uchaguzi yametengeluliwa.
Kanda ya Dar es Salaam, Omari Abdulkadiri rufaa ya yake imeshindwa na hivyo maamuzi ya kamati ya uchaguzi yamebaki kama yalivyo.
Faridi Mbaraka Salim Nahdi rufaa yake imeshindwa kwa kushindwa kutofautisha miaka yake ya kuzaliwa kati 1996 na kuonekana amezaliwa 1972 .
Eliudi Peter Mvela rufaa yake imeshindwa kwasababu ya kutokuwajibika kwenye kamati ya utendaji alipashwa kutetea kile walicho kubaliana ndani ya kamati ya utendaji kwa mujibu wa ibara 36 ya katiba ya tff na ibara ya 12(b)(d).
Kanda ya Shinyanga Mbasha Matutu rufaa yake imeshindwa kwani imethibitika alishiriki kutaka wenzake washindwe, hivyo alikosa uadilifu.
Mwenyekiti wa bodi Ahmed Yahya aliwekewa pingamizi kuwa yeye si mwenyikiti halali wa Mtibwa Sports klabu , kamati imeaangalia katiba ya Mtibwa imeonekana kuwa aliaacha madaraka na baadaye kuteuliwa na bodi badala ya uchaguzi halali hivyo kamati imebaini kuwa si mwenyekiti wa halali wa Mtibwa.
 Rufaa yake Michael Richard Wambura imeshindwa kwasababu ya kutokuwa na sifa ya kugombea nafasi hiyo, na kwamba maamuzi yaliyotolewa na kamati ya rufaa ya jaji Mkwawa yamesimama kama yalivyokuwa kwani ilimuona kuwa si muadilifu na kwamba kwa mujibu wa ibara 9 ni kwamba Wambura alitakiwa kudai haki yaki yake kupitia mahakama ya michezo ya kimataifa (CAS), kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya kamati ya jaji Mkwawa.
Katika nafasi ya Rais, mkata rufaa Omari Mussa Mkwaruro rufaa yake imeshindwa kutokana na kuonekana kutokuwa na kutokujua vizuri mambo ya soka ikiwa ni kushindwa kujibu sawasawa maswali ya kamati ya rufaa.
Mkwarulo alishindwa kujibu hata swali la mipango yake ya baadaye endapo atashinda kiti cha Rais wa TFF, hivyo kamati imeona udhaifu mkubwa wa upeo wake katika masuala ya soka na katiba ya TFF.
Kwa upande wa rufaa aliyokatiwa Jamali Emily Malinzi, Yeye amekosa uzoefu kushughulikia masuala ya soka kwa miaka 5 licha ya kwamba kuna ushahidi kuwa alikuwa katibu wa Yanga kutoka 2003 mpaka 2006 mwenyekiti wake alikuwa Fransis Kifukwe lakini hajatimiza miaka 5.
Ushahidi mwingine ni kuwa yeye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera na ameupata mwaka jana lakini hajatimiza miaka na pia hakuna ushahidi mwingine wowote ulionyesha kuwa amekuwa kiongozi wa soka sehemu nyingine yoyote.
Pili katika suala la uadilifu kuna taarifa kuwa Malinzi alipinga kuunga mkono maamuzi na maagizo ya shirikisho la soka duniani FIFA kutaka mabadiliko katika katiba ya TFF jambo ambalo lilikuwa ni maagizo ya FIFA ilhali akiwa kiongozi wa soka wa mkoa wa Kagera ambao ni wanachama wa TFF.

No comments:

Post a Comment