Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya Diesel na Edun.
Kampeni hiyo inayoitwa Diesel + Edun ilianzishwa
mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni hiyo, Renzo Rosso - na
waanzalishi wa kampuni ya Edun , Ali
Hewson na Bono walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa
pamba barani Afrika.
Flaviana Matata akiwa huku majuu akifanya vitu vyake
Waanzilishi
hao waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya
wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo
hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Flaviana Matata
Nguo hizo
zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini
Marekani na duniani. Pia nguo za Diesel + Edun zitauzwa kupitia mitandao
mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Compass Communications Limited, Maria Sarungi Tsehai
amesema kuwa Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki
kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni
za nguo hizo.
No comments:
Post a Comment