TAARIFA KWA UMMA
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL
BOARD)
04/02/2013
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu
wananchi wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na
Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:
1.
TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD
(a)
Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi
walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
INAYOGOMBEWA
|
S/N0.
|
JINA
|
MWENYEKITI
WA TPL BOARD
|
1.
|
Hamad
Yahya Juma
|
2.
|
Yusufali
Manji
|
|
|
|
|
MAKAMU
MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Said
Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
|
MJUMBE
–KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)
|
1.
|
Kazimoto
Miraji Muzo
|
|
2.
|
Omary
Khatibu Mwindadi
|
(b)
Mwombaji
uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za
uendeshaji za TPL Board Ibara ya 28(2) kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya
Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya
Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.
2.
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
(a)
Waombaji
uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa
hapa chini:
NAFASI
|
S/No.
|
JINA
|
RAIS
WA TFF
|
1.
|
Athumani
Jumanne Nyamlani
|
2.
|
Jamal
Emily Malinzi
|
|
MAKAMU
WA RAIS WA TFF
|
|
|
2.
|
Ramadhan
Omar Nassib
|
|
3.
|
Wallace
Karia
|
|
MJUMBE
WA KAMATI YA
UTENDAJI
–
Kanda
ya 1 (Kagera, Geita)
|
|
|
1.
|
Kalilo
Samson
|
|
2.
|
Salum
Hamis Umande Chama
|
|
|
|
|
Kanda
ya 2 (Mwanza, Mara)
|
1.
|
Jumbe
Oddessa Magati
|
2.
|
Mugisha
Galibona
|
|
3.
|
Samwel
Nyalla
|
|
4.
|
Vedastus
F.K Lufano
|
|
|
|
|
Kanda
ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
|
1.
|
Epaphra
Swai
|
|
|
|
Kanda
ya 4 (Arusha, Manyara)
|
|
|
1.
|
Elley
Simon Mbise
|
|
2.
|
Omar
Walii Ali
|
|
|
|
|
Kanda
ya 5 (Tabora, Kigoma)
|
1.
|
Ahmed
Idd Mgoyi
|
2.
|
Yusuf
Hamis Kitumbo
|
|
|
|
|
Kanda
ya 6 (Rukwa, Katavi)
|
|
|
1.
|
Blassy
Mghube Kiondo
|
|
2.
|
Seleman
Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti
vyake)
|
|
|
|
|
Kanda
ya 7 (Iringa, Mbeya)
|
1.
|
David
Samson Lugenge
|
2.
|
John
Exavery M. Kiteve
|
|
3.
|
Lusekelo
E. Mwanjala
|
|
|
|
|
Kanda
ya 8 (Ruvuma, Njombe)
|
1.
|
James
Patrick Mhagama
|
2.
|
Stanley
W. D Lugenge
|
|
|
|
|
Kanda
ya 9 (Mtwara, Lindi)
|
1.
|
Athuman
Kingome Kambi
|
2.
|
Francis
Kumba Ndulane
|
|
3.
|
Zafarani
Mzee Damoder
|
|
|
|
|
Kanda
ya 10 (Dodoma, Singida)
|
1.
|
Hussein
Zuberi Mwamba
|
2.
|
Stewart
Ernest Masima
|
|
|
|
|
Kanda
ya 11 (Morogoro, Pwani)
|
|
|
1.
|
Riziki
Juma Majala
|
|
2.
|
Twahil
Twaha Njoki
|
|
|
|
|
Kanda
ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
|
1.
|
Davis
Elisa Mosha
|
2.
|
Khalid
Abdallah Mohamed
|
|
3.
|
Kusianga
Mohamed Kiata
|
|
|
|
|
Kanda
ya 13 (Dar es salaam)
|
1.
|
Alex
Crispine Kamuzelya
|
2.
|
Juma
Abbas Pinto
|
|
3.
|
Muhsin
Said Balhabou
|
(b)
Waombaji
uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama
ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i) Ndg.
Omary Mussa Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF
hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7)
kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi
anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(ii)
Ndg. Michael Richard Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa
Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF
ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya
2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti
wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya
Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya
Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.
(iii)
Pia Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu
uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya
29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu
wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF haina
mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi
hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo
(CAS).
(iv)
Ndg. Abdallah Hussein Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya
Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na
ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa
kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(v) Ndg.
Mbasha Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu) hakukidhi matakwa ya Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa
Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.
(vi)
Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya
Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya
Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.
(vii)
Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba
ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka awe na uzoefu wa
uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia
hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu
na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya
TFF.
(viii)
Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa
ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa
sehemu ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.
(ix)
Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba
ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa
kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya
Katiba.
(x) Ndg.
Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri
wake na vyeti vya elimu havikubaliani.
(xi)
Ndg. Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya
Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa hakuhudhuria usaili.
(xii)
Ndg. Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi
matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya
TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania
(FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa
FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
(xiii)
Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya
Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye
uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha
umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi.
Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
3.
Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji
uongozi wa TFF na TPL Board.
4.
Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF
utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.
Deogratias
Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI
YA UCHAGUZI TFF
No comments:
Post a Comment