Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI na Kiongozi wa Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Luizer Mbutu anataraji kufanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday Party) siku ya Jumamosi tarehe 09-02-2013 katika ukumbi wa Mango Garden uliopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Luizer Mbutu hii ni mara ya pili kufanyiwa sherehe hiyo
huku kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana, sherehe ilifanyika katika Club
ya Maisha iliyopo Oysterbay.
Luzer Mbutu
Ikumbukwe ASET Imeamua kumfanyia Luizer Mbutu sherehe
hiyo kwa mara yapili mfululizo kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa katika
bendi ya Twanga Pepeta kwa kudumu kwa muda mrefu bila kuhama na kwa kufanya
kazi kwa kujituma bila ya kuchoka toka aanze kazi rasmi ndani ya Bendi mpaka
leo.
Luizer Mbutu akiwajibika
Sambamba na sherehe hiyo Twanga Pepeta kama ilivyo
kawaida yao watainogesha sherehe hiyo ya Kiongozi wao kwa masebene matamu
yatayoendana na nyimbo nzuri zilizo na meseji zilizojitosheleza kutoka kwa
wanamuziki wenye vipaji vya viwango vya hali ya juu kabisa.
Wadau mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe hiyo ili
kutoa sapoti kwa Kiongozi huyo wa Bendi katika siku yake ya kuzaliwa kwa kuwa
utatumika utaratibu kama wa mwaka jana wa kulishwa keki kwa wadau na marafiki
walio karibu na bendi ya Twanga Pepeta.
No comments:
Post a Comment