Saturday, February 16, 2013

Drogba aanza vitu vyake Galatasaray, acheka na nyavu

ISTANBUL, Uturuki
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, amewakumbusha Chelsea, makali yake baada ya kupiga bao katikam mechi yake ya kwanza akiwa amevaa uzi wa Galatasaray, jana.
Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast, alifunga bao hilo katika mechi ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Akhisar Belediyespor, likiwa bao lake la kwanza barani Ulaya tangu alipofanya hivyo, katika mechi ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka jana.
Kwa mtindo wake uliozoeleka, Drogba alirukja juu na kuifungia Galatasaray bao hilo dakika ya 68.
Mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Chelsea msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la FA na Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012.
Drogba aliitumikia Chelsea kwa muda wa miaka nane na kuihama msimu uliopita, baada ya kushindwa kuongezwa mkataba aliokuwa akiutaka.
Uamuzi wa mshambuliaji wa Atletical Madrid,  Radamel Falcao’, kuamua kubaki katika klabu yake, umekuwa mzuri, huku Fernando Torres, akipigania kurejesha makali yake aliyokuwa nayo wakati akiitumikia Liverpool.
Mashabiki wa Chelsea wanaona bora mshambuliaji wao wa zamani, Drogba,  angeendelea kubaki katika klabu hiyo na kuwapa raha.

No comments:

Post a Comment