SIMBA YAREJESHWA UONGOZI WA LIGI KUU YA VODACOM KWA YANGA BAADA YA KUTANDIKWA BAO 2-0 NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA JAMHURI MOROGORO
Mshambuliaji
wa Klabu ya Simba Emmanuel Okwi katikati akitafuta mbinu ya kuwatoka
wachezaji wa Mtibwa Sugar, Jamali Simba kulia na Hussein Ramadhani
kushoto wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwenye uwanja wa
Jamhuri mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar ilishinda bao 2-0. Picha kwa niaba ya www. fullshangwe.blogspot.com
Mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Ghana anayekipiga klabu ya Simba , Daniel
Akuffo mbele akijaribu kumilimi mpira dhidi ya mlinzi wa Mtibwa Sugar
wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo katika mchezo huo
ulimalizika kwa Simba kulala kwa bao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani
Morogoro.
Mwamuzi
wa kati Judith Gamba kutoka Arusha (mwenye mpira) akiwaongoza wachezaji
wa klabu ya Mtibwa Sugar Manungu Turiana na Simba katika mchezo wa ligi
kuu ya vodacom Tanzania bara uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Nahodha wa Klabu ya Simba Juma Kaseja akiwaongoza wachezaji wenzake kuwasalimia wachezaji wa Mtibwa Sugar.
Benchi
la ufundi la klabu ya Mtibwa Sugar likiongozwa na kocha mkuu wa klabu
hiyo Meck Mexime kulia muda mfupi kabla ya vijana yake kuiadhibu Simba
kwa kuwapakipigo cha bao 2-0 katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara
kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Benchi
la ufundi la klabu ya Simba likiongozwa na kocha mkuu Milovan Cirkovic
kushoto muda mfupi kabla ya timu yake kupokea kipigo cha bao 2-0 katika
ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa
Jamhuri mkoani Morogoro
Jukwaa la klabua ya Simba wakiwa wanafuatilia mchezo baina ya timu yao na Mtibwa Sugar baada ya kupokea kipigo cha bao 2-0.
Sehemu
ya jukwaa la wazi la mashabiki mchanganyiko nao wakifuatilia mchezo huo
ambao umeishia kwa Simba kukubali kufungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar.
No comments