Wahudumu wa baa kupata mafunzo maalum ya kuwahudumia wateja wanaokunywa whiski
WAHUDUMU mbalimbali wa baa
nchini, leo watapata mafunzo maalum ya jinsi ya kuwahudumia wateja wanaotumia
pombe kali (whiski) kutoka kwa balozi wa balozi wa kinywaji cha Glenmorangie,
Niel Hendriksz.
Mafunzo hayo yanalenga upatikanaji
wa huduma bora sambamba na uchanganyaji wa kinywaji hicho kwa lengo la
kuwafanya wanywaji kupata kinywaji kilicho bora kwa afya zao.
Akizungumza jijini jana, Hendriksz
ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku mbili alisema kuwa wameamua kufanya
mafunzo hayo ili kuboresha huduma zao na ni njia moja ya kuboresha soko la
kinywaji hicho hapa nchini.
Alisema kuwa bidhaa zao
zinatengenezwa nchini Scotland, na wamedumu kwa kipindi kirefu katika soko na
sasa wameamua kuongeza nguvu kwa upande wa hudhuma.
Mbali na kutoa mafunzo hayo, barozi
huyo atawaelimisha wahudumu hao juu ya uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji hivyo
katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa kwenye ziara ya siku
tano katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo hapa nchini atakuwa kwa
siku mbili na maunzo mengine atayatoa nchi nyingine.
Alifafanua kuwa atakutana na makundi
tofauti ya utoaji wa huduma ya kinywaji chao mbali ya wafanya boashara mbali
mbali lwa lengo la kudumisha soko.
“Kutakuwa na nafasi 20 kwa nchi
nzima kuhudhuria mafunzo ambapo pia tutabadilishana mawazo na watu mbali mbali
ambao ni wadau wa kinywaji chetu," alisema.
Ziara ya Hendrisksz inatarajia
kumalizika keshokutwa ambapo ataelekea nchini Nairobi kwa mwendelezo wa
ziara hiyo Afrika Mashariki.
No comments