Shabiki Leeds atupwa jela kwa kumpiga kofi kipa uwanjani
![]() |
Aaron Cawley |
LEEDS, England
SHABIKI wa timu ya Leeds United, ya
England aliyemvamia kipa wa Sheffield Wednesday, Chris Kirkland, amefungwa wiki
16.
Aaron Cawley mwenye miaka 21, kutoka
Cheltenham, alikiri kuvamia na kushambulia wakati wa mechi ya Sheffield
Wednesday dhidi ya Leeds, iliyochezwa Ijumaa usiku katika uwanja wa nyumbani wa
Sheffield.
Cawley, aliyehudhuria mahakama ya Sheffield, alikamatwabaada
ya kipa wa Wednesday, Kirkland kusukumwa kichwani wakati wa mechi hiyo
iliyopigwa Hillsborough.
Kirkland, aliyewahi kuichezea timu
ya England, alianguka chini baada ya tukio hilo, kufuatia bao la kusawazisha
dakika ya 76.
Cawley alionekana kwenye kamera akikimbia
kutoka upande wa mashabiki wa Leeds na kuingia uwanjani na kumsukuma Kirkland
usoni, kabla ya kurejea tena kwa mashabiki wenzake.
Macaulay alisema Cawley, aliwaambia
maofisa kuwa, alilewa sana Ijumaa asubuhi, robo tatu ya pombe aina ya vodka,
kabla ya kupanda treni kuelekea Sheffield.
Taarifa ya kwenye mtandao wa Leeds
ilisema: Msemaji wa klabu alisema: "Tumefurahishwa kuona suala hili
limeshughulikiwa na mahakama kwa haraka. Tunepata taarifa kuwa, amehukumiwa
kwenda jela siki sita na kufungiwa miaka mitano.
No comments