Header Ads

ad

Breaking News

Serengeti Boys yaitwa Mbeya


Serengeti Boys


TIMU ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, imeondoka jana kwenda mkoani Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Soka mkoani humo (MUFA), ikiwa ni maandalizi ya mechi ya kufuzu fainali za vijana za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Awali, Serengeti Boys ilitakiwa kucheze na Kenya, mechi ya kwanza, lakini timu hiyo ilijitoa kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa, MUFA wataihudumia timu hiyo kuanzia malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo mpaka itakaporejea Dar es Salaam, kuendelea na kambi.

Alisema Serengeti Boys iliyo chini ya Jakob Michelsen akisaidiwa na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, ipo katika maandalizi ya mechi dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Misri.

Wambura alisema kuwa, timu itapangiwa michezo ya majaribio na timu za mkoani humo, ikiwemo Mbeya City, Tanzania Prisons na kombaini.

Aliongeza kuwa, TFF inatoa shukrani na pongezi kwa MUFA, kwa kuonesha mfano wa kuigwa na wadau wengine wa michezo, kushirikiana katika maandalizi ya kuziandaa timu za taifa.

“Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa MUFA, na kuwasihi wadau wenginne wa soka nchini kuiga mfano huo kwa kuzisaidia timu zetu za taifa, kwani kufanya hivyo, tutaonesha uzalendo, uwajibikaji na kuguswa katika masuala haya,” alisema Wambura.

Wambura aliishukuru benki ya NMB kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo na fedha sh. milioni 5, ambazo zimewawezesha vijana wa timu hiyo kupata posho zao za kambi na usafiri wa kwenda Mbeya.

Alisema kuwa, Benki ya NMB imekuwa na mchango mkubwa katika soka la vijana kwa muda mrefu, na kwa kipindi cha miaka sita iliyopita, ilidhamini mafunzo ya makocha wanaojihusisha na maendeleo ya soka kwa vijana nchini.

No comments