Mama Karume awaongoza Yanga bungeni leo
Yusf Manji (kulia), akiapishwa na Jabir Katunda, kuongoza Yanga kama Mwenyekit. |
Mama Fatma Karume |
Wanachama wa Yanga wakifuatilia kuapishwa kwa viongozi wao. |
Kombe la Kagame limetinga Mjengoni muda mchache
uliopita na kulitikisa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya
utambulisho uliofanywa na Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Anna Makinda. Alianza kwa kusema.
“Tunao Wageni Mashuhuri walioiletea Sifa Nchi
yetu kwa kutwaa Kombe la Afrika ya Mashariki na Kati Maarufu kama Kombe la
Kagame mara mbili Mfululizo tena kwa KISHINDO siku chache zilizopita ndani ya
Uwanja Mpya wa Taifa Pale Dar es Salaam ambao ni Timu ya YANGA.
Timu hii
imeongozwa na Mama yetu Mke wa Muasisi wa Muungano Mama yetu Bi. Fatma Karume
Mama Karibu sana na nimefurahi kukuona ukiwa bado na afya tele. Pamoja na Mama
Karume pia ameandamana na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga Eng. Francis
Mponjoli Kifukwe (Makofi Mengi), Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Ndugu Yusuph
Mehboob Manji (Makofi Mengi Sanaaaaaaaaaaaaaaa), Makamu Mwenyekiti Ndugu
Clement Sanga (Makofi) pamoja na viongozi wengine waandamizi na Wazee wa Yanga
wakiongozwa na Mzee Akilimali.
Pia tunao wachezaji wote wa Yanga kama
mnavyowaona wakiwa kwenye nguo zao zinazopendeza za Njano wote kwa ujumla
simameni…. (Bunge lazizima kwa Ndelemo na Vifijo huku Captain wa timu hiyo
Carnavaro ainua Kombe juu). Spika aliendelea najua Mheshimiwa Spika Mstaafu
Samwel Sitta amenuna sana lakini hiyo ndiyo hali halisi na hata Simba wakija na
kombe nitawatangaza… (Vicheko Bungeni)…..
Tunawakaribisha sana na tunawatakia
kila la kheri kwenye shughuli zenu za kuijenga klabu yenu ili mtuletee furaha
zaidi siku zijazo jambo ambalo tunaimani linawezekana (Makofi mengi sanaaa na
Sauti ya Mheshimia Nasari ilisikika kwa mbali ikisema Tano bila Kichekooooo na
makofi ya kuipongeza Yanga yaliendelea na kumfanya Spika Acheke na kuwataka
Wabunge kuwa watulivu ili shughuli nyingine ziendelee).
aada ya Spika kukamilisha zoezi la
kuikaribisha Yanga Mjengoni Spika alimuita Mheshimiwa Bernard Camilus Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa awasilishe Hotuba yake.
Katika utangulizi wake Mheshimiwa Membe alisema “Nimefurahishwa na Ujio wa
Yanga humu ndani wakati wa Hotuba yangu kwakuwa name ni mdau mkubwa wa Timu
ya Yanga Hongereni kwa ushindi wa Kagame (Makofi mengiii)” Mwisho wa kunukuu.
Fuatana na www.mwanatanga.blogspot.com
kwa habari zaidi na zakina muda mchache ujao kuhusu kutinga kwa Kombe la
Kagame MJENGONI leo 06/08/2012.
Baada ya Spika kukamilisha zoezi la
kuikaribisha Yanga Mjengoni Spika alimuita Mheshimiwa Bernard Camilus Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa awasilishe Hotuba yake.
Katika utangulizi wake Mheshimiwa Membe alisema “Nimefurahishwa na Ujio wa
Yanga humu ndani wakati wa Hotuba yangu kwakuwa name ni mdau mkubwa wa Timu
ya Yanga Hongereni kwa ushindi wa Kagame (Makofi mengiii)” Mwisho wa kunukuu.
Fuatana na www.mwanatanga.blogspot.com
kwa habari zaidi na zakina muda mchache ujao kuhusu kutinga kwa Kombe la
Kagame MJENGONI leo 06/08/2012.
|
No comments