Luka Modric kupimwa afya Real Madrid leo
![]() |
Luka Modric |
LONDON, England
Tottenham imekubali kuwauzia Real
Madrid kiungo wao Luka Modric, ada ya puani milioni 30.
Mchezaji huyo kutoka Croatia mwenye
miaka 26, leo atakwenda Hispania kupimwa afya.
Tottenham, pia imetangaza kuingia
ushirikiano na klabu ya Real Madrid.
Makubaliano hayo yatazifanya klabu
hizo mbili kufanya kazi pamoja ikiwemo wachezaji , makocha na uhusiano wa
kiabishara.
Modric alijiunga Tottenham mwaka
2008 kwa pauni milioni 16.5, akitokea katika klabu ya Dinamo Zagreb ya Croatia.
No comments