Header Ads

ad

Breaking News

Kalala arejea Twanga na kurusha dongo Mapacha watatu

* Asema Koti lilimbana Mapacha na kuamua kulivua...
* Aibuka na  wimbo mpya "Nyumbani ni nyumbani"
* ASET yasema Amsha Amsha ndiyo kwanza imeanza!
Na Mwandishi wetu
UONGOZI wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Mapacha Watatu.
Kalala Junio akisindikizwa na baadhi ya wanenguaji wa bendi ya African Stars  kabla ya kutambulishwa na uongozi wa ASET kwa waandishi wa habari.
Mwimbaji huyo maarufu alisema kwa  fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao  kwa sasa upo katika hatua ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka  kuamua kurejea Twanga,”  alisema Kalala.
Kalala Junior akisisitza jambo mara baada ya kutambulishwa na Afisa Uhusiano wa ASET, Mohamed Pizaro kwenye ukumbi wa Mango Garden, kulia ni kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza

Alisema kuwa  ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka  fadhira za ASET ambapo ndipo alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba  wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki wengi wa muziki wa dansi.
Kalala Junior akitambulisha wimbo wake mpya, Nyumbani ni Nyumbani ambao umeenda sambamba na staili mpya ya unenguaji kama ilivyoonyeshwa na wacheza shoo wa Twanga Pepeta kutoka kulia, Sabrina, Mary na Sharapova
Afisa Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani ni Nyumbani .
Pizaro alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa wanatumikia bendi nyingine.
Kalala Junior akionyesha kipaji chake cha kucharaza drums

Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
Hapa Kalala akionyesha uwezo wake katika kucharaza gitaa la Bass
Karibu nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza.
Kiongozi Msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza akionjesha moja ya vionjo ya wimbo mpya wa Nyumbani Nyumbani wakati wa utambulisho wa Kalala Junior.


No comments