Kagera Sugar kucheza mechi nne za kirafiki
KOCHA msaidizi wa timu ya Kagera Sugar, Mlage
Kabange, amesema kwamba, wanahitaji mechi nne za kirafiki ili waweza
kukamilisha program yao, kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Kabange, amesema kwamba, baada ya kusongezwa mbele ligi
hiyo, wanahitaji mechi nne ili kukiimarisha zaidi kikosi chao.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wiki hii
lilitangaza kusogeza mbele ligi, hadi Septemba 15, mwaka huu, ikiwa ni mechi ya
Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na Azam FC, iliyokuwa ifanyike Agosti 25.
“Tumerudi kutoka Shinyanga, huko tumebahatika kucheza
mechi mbili, sasa hivi tunaendelea na mazoezi, lakini baada ya kusongezwa mbele
ligi, tukipata mechi nne za kirafiki, tutakuwa tumemaliza kazi,” amesema
Kabange.
Almeema kuwa, walikuwa na mpango wa kwenda Uganda
kucheza mechi za kirafiki, lakini ratiba imekuwa tofauti kwani timu za Uganda,
ziko kwenye mapumziko.
Kabange alisema kwamba, wapo kwenye mipango ya
kutafuta mechi hizo ili kuweza kuangalia makosa yao, kabla ya kuanza Ligi.
No comments