ZAWADI ZAMWAGWA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu mstaafu
Frederick Sumaye ameeleza kusikitishwa kwake na kupoteza umaarufu wa
soka la Tanzania kwa sasa ukilinganisha na miaka ya 1970.
Sumaye alisema hayo
juzi katika hoteli ya Double Tree By Hilton ya jijini Dar es Salaam
katika hafla ya kuwatunuku washindi mbalimbali waliofanya vema kwenye
ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012.
Alisema hali hiyo
inatokana na timu vilabu nguli vya Simba na Yanga kubweteka kwa moja
kuifunga nyenzake na kujiona zimefika peponi kitu ambacho si dalili
nzuri katika maendeleo ya soka.
“Simba kuifunga Yanga
au Yanga kuifunga Simba si kigezo kizuri cha kujiona ni timu nzuri, timu
inatakiwa iangalie ushindani kimataifa …ndiyo maana hata wakipangiwa
timu kutoka Misri, Ivory Coast n.k mnaingiwa na hofu kubwa,”alisema.
“zamani vilabu vya nje
vilikuwa vikipangwa na timu za Tanzania zinatetemeka lakini sisi
sasa…kama tunataka kurudi katika heshima yetu ya zamani tujipange
kimataifa, “aliongeza Sumaye.
Aidha, Sumaye
alisikitishwa na migogoro katika vilabu na kusema inachangia pia
kudidimiza soka hivyo amewataka viongozi kuhakikisha wanafanya kazi kwa
ushirikiano sambamba na kuvihudumia ipasavyo vilabu vyao. FULLSHANGWE
No comments