Rais Kikwete na mama Salma wahudhuria miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais
Paul Kagame wa Rwanda wakipokea haeshima za marais muda mfupi baada ya Rais
Kikwete kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali kuhudhuria
maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda leo asubuhi.
Rais dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakikagua gwaride la heshima katika uwanja wa ndege wa Kigali. |
Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa michezo wa
Amahoro mjini Kigali Rwanda kwaajili ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Rwanda.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais
Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru
wa Rwanda zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amahoro jijini Kigali leo
asubuhi(picha na Freddy Maro)
No comments