Wakali wa Epiq BSS Lindi waanikwa
![]() |
Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen akimfariji mshiriki mmoja wa washiriki wa shindano hilo aliyekosa nafasi ya kuchaguliwa. |
Mwanadada ahuyu alikuwa mmoja kati ya waliojitokeza kushiriki katika
kinyang’anyiro cha kuwatafuta wakali wa Lindi.
Na Mwandishi Wetu
PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS
2012) mkoa wa Lindi limefungwa ambapo washindi watano tayari wamepatikana.
Msako huo wa vipaji mkoani hapa ulifanyika kwa siku
mbili mfululizo ambapo vijana wengi walijitokeza kuonesha vipaji vyao
kiasi cha kuwapelekea majaji kuwa na wakati mgumu kupata wawakilishi.
Akizungumzia mchakato wa Lindi Jaji Mkuu wa EBSS
2012 Ritha Paulsen alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kuanza kwa shindano
hilo mkoani hapa ameridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza.
Alisema kuwa EBSS 2012 ilifanya uamuzi wa kutafuta
vipaji mkoani Lindi ili kuwapatia nafasi washiriki wa Lindi kuonesha
uwezo wao wa kuimba aina mbalimbali za nyimbo.
“Mkoa wa Lindi ninaamini kuwa ni kati ya mikoa
ambayo kuna vipaji vingi vilivyojificha hivyo EBSS kazi yetu ni kuwatengenezea
njia ya kufikia mafanikio yao, sasa tukipata vipaji hivi kitakachobakia
ni wao kuonesha uwezo wao”alisema Ritha.
Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya
simu ya Zantel ambao ni wadhamini wa EBSS 2012, Awaichi Mawalla mbali
na kuridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza alielezea umuhimu wa sanaa
katika kuinua uchumi wa mkoa wa Lindi.
“Hii ni nafasi ya kipekee kwa wakazi wa mkoa huu
kujitengenezea ajira kupitia muziki, kama inavyofahamika kuwa Zantel
imejikita katika kurahisisha maisha ya watu wote sasa kwa kuona umuhimu
wa muziki katika kukuza ajira imeamua kujikita katika muziki kwa maendeleo
ya vijana” alisema Awaichi.
No comments