WAZIRI MKUU ATAKA ALAT IKUNJUE MAKUCHA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magu,
Jaqueline Liana baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza
ambako alifunga sherehe za maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa
kitaifa kwenye uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza Julai 1, 2012.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhandishi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Ataka iache
kukaa kimya, ikemee uozo kwenye Serikali za Mitaa
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka
Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) iache kukaa kimya na badala yake ikemee uozo unaofanywa na watendaji
kwenye Serikali za Mitaa nchini.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumapili, Julai mosi, 2012) wakati akifunga maadhimisho ya nane ya Siku ya
Serikali za Mitaa yaliyofanyika kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu alisema kwa
mujibu wa Katiba ya ALAT, Jumuiya hiyo inao wajibu wa kuzisimamia Halmashauri
kwa iliundwa ili kudumisha
na kukuza maendeleo ya shughuli za Serikali za Mitaa Tanzania kwa kuondoa vikwazo
na matatizo yote.
“Serikali za Mitaa
zinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa nilizozianisha ni ukusanyaji
mdogo wa mapato, usimamizi duni wa matumizi ya fedha na baadhi ya Halmashauri
kushindwa kupata ruzuku ya maendeleo,” alisema.
Akizungumzia kuhusu
ukusanyaji mdogo wa mapato, Waziri Mkuu alisema uko chini licha ya Halmashauri
nyingi kuonesha kuwa zingekusanya mapato na kuongeza vyanzo vya mapato.
No comments