Wanyange 15 wajitokeza Sinza
Miss Sinza |
Na Mwandishi Wetu
WANYANGE 15
wamejitokeza kuwania taji la Mrembo wa Sinza “Redds Miss Sinza 2012”
yaliyopangwa kufanyika julai 13 kwenye ukumbi wa Mawela social (Ten Star
Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican City.
Mratibu wa mashindano
hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment, aliwataja warembo hao ni
Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi na Vailet
John.
Wengine ni Esther Mussa,
Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi,
Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Omary alisema kuwa,
warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma, ambaye kwa sasa
anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model.
Alisema kuwa, mazoezi ya warembo hao
yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30
mchana.
“Warembo wamepania
kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano na hii inatokana na ukweli kuwa,
wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu vidogo vidogo vya
mashindano hayo, alisema Majuto.
Alisema lengo la
mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania, mbali ya taji la
Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold,
Dodoma Wine na Kidoti Fashion.
Wadhamini wengine ni
Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P,
Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics
Kinondoni.
“Tuna warembo moto wa
kuotea mbali ambao kwa sasa wameonesha kupania kufanya kile ambacho kinachosubiliwa
na wadau wa urembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake, hii inatokana na
ukweli kuwa, mashindano haya ni ya
mwisho kwa upande wa vitongoji jijini,” alisema.
Miss Sinza |
No comments