WAAMUZI 15 WATEULIWA KUCHEZESHA KOMBE LA KAGAME
![]() |
Boniface Wambura, Msemaji TFF |
Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua
waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini
Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi
hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya
vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12
na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa
CECAFA.
Kwa
upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony
Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara),
Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali
(Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
No comments