MISRI YAAHIRISHA MECHI DHIDI YA NGORONGORO HEROES
Mechi mbili za
kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka
20 (Ngorongoro Heroes) na Misri zilizokuwa zichezwe mwezi huu zimefutwa.
Chama cha Mpira wa
Miguu Misri (EFA) kimetuma taarifa jana (Julai 1 mwaka huu) kikiomba kusogezwa
mbele hadi mwishoni mwa Agosti baada ya kushindwa kupata usafiri wa ndege
kuwahi tarehe ambazo ilikubaliana na TFF kwa ajili ya mechi hizo.
Ngorongoro Heroes
ambayo tayari iko kambini ilikuwa icheze mechi hizo Julai 3 na 5 mwaka huu
jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Nigeria
katika mechi ya michuano ya Afrika, Julai 29 mwaka huu.
Mechi nyingine za
kirafiki kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Jakob Michelsen zitachezwa
Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
No comments